Dar IVF & Fertility Clinic
We make families complete

Ninawakaribisha kwenye kliniki yetu mpya. Ninawaletea uzoefu wangu wa matibabu ya uzazi nilioupata kutoka Uingereza, Kuwait na Uganda. Huu uzoefu ni wa asili na ulitokana na msukumo kutoka kwa mama yangu mzazi Mganda, ambaye alikuwa mkunga wa jadi. Nilikuwa nasaidiana naye katika kutoa huduma ya uzazi kwa kina mama aliyokuwa akiifanyia nyumabani kwetu Masaka.

Naamini kwa msaada wa Mungu na wa wafanyakazi wetu wa kliniki ya Dar ambao wamebobea na kujizatiti katika kazi yao, itasaidia wanandoa wengi kupata mtoto baada ya kuwa wamekuwa wakijaribu kuwa na familia kwa miaka mingi bila ya mafanikio.

Naweza kusema kwamba hatuwezi kusaidia kila mtu ambaye ataingia milango ya kliniki yetu. Ila kwa muongozo mzuri na kujua tatizo, pamoja na motisha, subira na msaada wa kifedha,  naamini wanandoa wengi wana nafasi nzuri sana ya kupata mtoto.

Mtoto wa kwanza kuzaliwa kutumia teknologia ya IVF (upandikizaji) katika Dunia ni Louse Brown ambaye alizaliwa mwaka 1979 nchini Uingereza. Tangu wakati huo, watoto zaidi ya milioni 6 wamezaliwa duniani kote. Watoto waliozaliwa kwa njia hii (IVF) ni wakawaida kabisa na hawana tofauti na watoto ambao mimba zao zilitungwa kwa njia ya asili. Kipindi cha ujauzito, mimba ni sawa na mimba ya kawaida. Watoto ni wakawaida na hakuna tofauti na wale mimba zao zilitungwa kawaida. Matukio ya kasoro ya kuzaliwa ni sawa na watoto ambao mimba zao zilitungwa kwa njia ya asili. Kama jambo la kweli,  ukiuliza akina mama ambao wamejifungua watoto kwa kutumia teknolojia ya IVF, ni jinsi gani watoto wao wanafanya mashuleni, wengi watakuambia kuwa watoto wao ni nadhifu kuliko wa majirani zao! Hii huenda inaonyesha kwamba nikupendwa zaidi kwa watoto hawa.

Mama yetu mkongwe kutoka Uganda alijifungua mtoto mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 62. Mama mkongwe katika ulimwengu wote alijifungua mtoto katika umri wa miaka 67. Yeye alijifungua watoto mapacha wa kike mwaka 1986 huko Romania kupitia teknolojia ya IVF. Bila shaka tunajua katika Biblia mama mkongwe Sarah alipata mtoto akiwa na umri wa miaka 90. Naamini Mungu alikuwa anajaribu kutuambia kuwa tukiamini na kuwa pamoja naye hakuna vikwazo vyovyote. Teknolojia hii ya IVF ni Mungu aliileta.

Kliniki yetu na Hospital ya wanawake na uzazi Uganda, ilikuwa ya kwanza kuwa na mtoto aliyezaliwa kutumia teknolojia ya IVF katika Afriaka Mashariki na Kati.Tunamshukuru Mungu kwa kuwa waanzilishi wa kwanza wa teknolojia hii katika ukanda huu.Tunajivunia kuwa wana Afrika Mashariki.

Tangu wakati huo, watoto zaidi ya 600 wamezaliwa kwa kutungwa mimba kwa njia ya teknolojia ya IVF katika kliniki yetu ya Kampala. Tumeweza kuwasaidia familia nyingi kutoka Tanzania kutimiza ndoto yao ya kuwa na watoto walipotutembelea kliniki yetu ya Kampala na kupata matibabu.

Hawa wanandoa wako tayari kutoa ushuhuda wao. Unaweza pia kuona baadhi ya picha za watoto wao kwenye nyumba yetu ya sanaa kwenye kliniki yetu.
Kliniki yetu ya Dar iko tayari kuongeza kasi na kushirikiana na madaktari wa ndani ya nchi kwa njia ya mafunzo ya semina ambayo itafanyika miezi ijayo kueneza teknolojia hii sehemu mbalimbali za Tanzania.

Si kila kesi ya utasa inahitaji ya teknolojia ya IVF. Kuna njia nyingine za kusaidia uzazi (ART) mbinu kama vile; Kudhibitiwa usisimuaji wa ovari, IUI (Uingizaji wa mbegu kwenye kizazi), Mbegu kuosha kwa wanandoa wenye VVU, ambayo inaweza kutumika katika kuchagua na kusaidia wanandoa tasa katika suala hili.

Mzigo wa Gharama

Teknolojia hii ni ya gharama kubwa katika suala la muda, msongo wa mawazo na hisia, mvutano wa familia kila upande, na suala la fedha.
Tunafahamu haya matatizo na sisi tuko tayari kutoa huduma za ushauri katika kesi ya kila mtu binafsi ili kuhakikisha kwamba wewe unapewa matibabu bora na yanatolewa kwa tatizo/hitaji lako maalumu.

Mwisho, nataka kukuhakikishia kwamba sisi tunatoa asilimia mia moja (100%) ya usiri juu ya mgonjwa na kesi yake. Sisi hatutazidhihirisha kwa mtu yeyote habari yoyote kuhusu matibabu yako hata kama umefanikiwa. Sisi pia tutachukua hatua kali za kinidhamu kwa mfanyakazi wetu yeyote ambaye atajaribu kutoa taarifa yako ya matibabu kwa mwanachama yeyote wa umma. Haya ni kabla ya mahitaji ya maadili matibabu ya kwamba sisi tuna kiwango kikubwa cha utii kwayo.

Huduma zetu

  1. Mashauriano
  2. Ultrasound ya kizazi
  3. Vipimo vya damu
  4. X-rays za mirija ya uzazi (HSG)
  5. Uchunguzi wa kizazi bila upasuaji (Hysteroscopy na Laparoscopy Surgery)
  6. Uchambuzi wa Manii

© 2024 Dar IVF, Fertility and Maternity Clinic Haki zote zimehifadhiwa.